March 3, 2021


MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa wana mipango mirefu na Kocha Mkuu wa timu hiyo Cedric Kaze hivyo bado yupo ndani ya kikosi hicho.

Hivi karibuni kumekuwa na presha kubwa kwa Kaze kutajwa kuwa amepewa mechi kadhaa ili aweze kuchimbishwa kutokana na kuwa na mwendo ambao hauridhishi.

Taarifa zimekuwa zikieleza kwamba mabosi wa Yanga wapo kwenye mpango wa kumfuta kazi kocha huyo ili waweze kuleta kocha mpya.

Kwenye mechi za mzunguko wa pili baada ya kuongoza kwenye mechi nne ambapo amekuwa na mwendo wa kusuasua.

Alianza kwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela, sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City na sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar.

Ameshinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na bao 1-0 dhidi ya Ken Gold kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora na timu hiyo imetinga hatua ya 16 bora.

Injinia ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhami wa Klabu ya Yanga, amesema:"Kaze yupo ndani ya Yanga kwa muda mrefu kwa kuwa ni mwalimu ambaye tumemwamini na hakuna ambaye anafikiria kuachana naye.

"Kuna timu nyingi duniani ambazo zimekuwa zikipata matokeo mabovu ikiwa ni pamoja na ile ya Liverpool ambayo inanonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen Klopp.

"Hivyo kupata matokeo mabovu haina maana kwamba Klopp ni mbovu, na timu yetu haijapata matokeo mabaya na haina matokeo mabovu kwa kuwa bado haijapoteza mechi yoyote ya ushindani," amesema.

Kwa sasa timu ipo Tanga na kesho ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mzunguko wa kwanza Yanga ilishinda mabao 3-0 hivyo kesho kila timu itakuwa inahitaji kuweka rekodi yake, Yanga kulinda na Coastal Union kutibua.

14 COMMENTS:

  1. Coastal piga hao vyura wapiteane jumla

    ReplyDelete
  2. Kama timu haaina matokeo mabovu sasa huo mfano wa Klop na Liverpool unakujaje

    ReplyDelete
  3. Ligi Bado sana kufukuza Coach sio solution ya kutibu matatizo, Big up kwa GSM wanajua wanachofanya ndio maana hawaendi kwa mihemko ya mikia

    ReplyDelete
  4. GSM au Yanga?Which is which?Nani sasa ana sauti ys kusema kuhusu kocha ?Mwenyekiti au GSM?
    Tumechukuliwa mateka na GSM wanayanga tuzibe midomo hatuna cha kufanya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe unaleta fitna na sio shabiki wa Yanga

      Delete
    2. Wew kama hayakuhusu pita kushoto

      Delete
  5. Kazi wanay kwamaan kila mech wao wana cheza kwa presha

    ReplyDelete
  6. et liverpool, kwani hao Yanga walicheza vizuri misimu miwili iliopita mpaka mjilinganishe na liverpool??? akili ndogo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Elewa kwanza ndipo ujibu usikurupuke huo ni mfano hajamanisha kwamba yanga na Liverpool ni sawa

      Delete
  7. Hii ndo yanga bwana, ina misimamo yake sio kama unavyoropoka wew. Yanga tuendelee kusonga mbele

    ReplyDelete
  8. Kaze hana muda mrefu atasepa

    ReplyDelete
  9. Wewe kama sio mwana yanga usichangie kwani hayakuhusu

    ReplyDelete
  10. Uamuzi wa kutofukuza kocha ni wa busara kwani tunapofikiria matokeo hasi tufikirie pia matokeo chanya. Suala hapa ni nani mweny kauli ya mwisho kati ya Yanga na GSM?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic