March 1, 2021


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mtego alioingia mchezaji wake Carlos Carlinhos umemponza kwa kadi aliyoonyeshwa jambo ambalo litaigharimu timu.

Raia huyo wa Angola alionyeshwa kadi hiyo ya kwanza baada ya kutua Bongo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho baada ya kuonekana akimpiga ngumi beki wa Ken Gold, Boniphance Mwanjonde.

Alitumia dakika 14 kwa kuwa aliingia akitokea benchi jambo ambalo limemvuruga Kaze katika kusaka mbadala wake.

Kaze Machi 4 ana kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani atakosa huduma ya kiungo huyo mwenye mabao matatu na pasi mbili ndani ya ligi.

Kaze amesema:-"Nimeongea naye ameonesha kujutia na ameomba msamaha kwa kosa lake , ninaona kwamba aliingia kwenye mtego kwa kosa lake la kumpiga mchezaji wa timu pinzani hivyo kwetu ni pigo kwa kuwa tutamkosa kwenye mechi zijazo.

"Tayari alikuwa amerejea kwenye ubora na alianza kufanya vizuri kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye majeraha hivyo alikuwa anarejea taratibu na kazi yake ilikuwa inaonekana.

"Kukosekana kwake ni kazi kwetu pia kujipanga kwa ajili ya wakati ujao na imani yetu ni kuona tunaweza kufanya vizuri bado nafasi ipo," amesema.

Baada ya kutinga hatua ya 16 bora mchezo wao ujao ni dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic