HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wachezaji wake wana kazi ya kuongeza juhudi kwa ajili ya kupata matokeo chanya kwenye mechi zao zijazo za mzunguko wa pili.
Mtibwa Sugari haijawa na mwendo mzuri ndani ya msimu wa 2020/21. Kwenye msimamo ipo nafasi ya 14 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 24.
Mchezo wao wa mwisho wa ligi ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Gwambina FC, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wanatambua mwendo ambao wanakwenda nao sio mzuri jambo ambalo ni lazima lifanyiwe kazi.
"Ushindani umekuwa mkubwa hilo lipo wazi na matokeo ambayo yanapatikana bado yamekuwa ni mabaya kwetu.
"Tunachotakiwa kwa sasa ni kuona namna gani wachezaji wataweza kufanya vizuri wakati ujao uwanjani kwenye mechi zetu, bado tuna nafasi ya kurekebisha pale ambapo tulikosea," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment