BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba amesema kuwa hakuna ugomvi wowote uliopo kati ya mchezaji wao, Bernard Morrison na kocha wa timu hiyo Didier Gomes.
Imekuwa ikielezwa kuwa, Gomes raia wa Ufaransa hayupo kwenye maelewano mazuri na nyota huyo raia wa Ghana ambaye anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.
Ndani ya ardhi ya Bongo alianza kukipinga ndani ya Yanga ambao wanadai ni mchezaji wao kwa kuwa dili lake la miaka miwili halikuisha na kesi yao kwa sasa ipo kwenye mahakama ya usuluhishi ya kimataifa, (Cas).
Hakuwa kwenye kikosi ambacho kilikwea pipa kueleka Sudan ambapo kilicheza jana, Machi 6 na kulazimisha sare ya bila kufungana mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Pia hakuwa kwenye kikosi kilichomenyana na JKT Tanzania, Uwanja wa Mkapa ulikuwa ni mchezo wa ligi jambo ambalo limepelekea habari hiyo kueleza kwamba hapo ndipo ugomvi wao ulianza.
Barbara amesema kuwa:"Hakuna ukweli kuhusu ugomvi wa kocha na mchezaji wetu Morrison hizo habari ni za uongo na hilo sisi tunajua kwamba si kweli.
"Alibaki Tanzania hilo lipo wazi ila ilikuwa ni kwa sababu za benchi la ufundi haina maana kwamba yupo na ugomvi na mwalimu,".







Wahuni wajitahidi kuzingatia mambo yao kama vile mechi za Tanga na Arusha. Wasihangaike na yasiyowahusu
ReplyDeletePale wasafi kwa kweli naona wanadhani wao ndio kila kitu kwenye tasnia za michezo. Wanafanya vizuri inafika pahala mpaka wanasahau majukumu yao mama ya kuwabarisha watu kwa usahihi na kukimbilia udaku na kuingilia kazi za watu wengine.Tetesi Kama tetesi basi Kama chombo Cha habari makini kilichotekabmasikio ya mamilioni ya wasikilizaji basi ni haramu kuzifanya tetesi kuwa habari kamili. Simba ya sasa tulikuwa tunalia kuwa timu zetu kutokuwa na mfumo mzuri wa utoaji wa habari na Siri za club ila Simba hii kitu Kama hujasikia kutoka kwa Manara au CEO Barbara basi ujue ni uzushi tu. sasa vipi kitenge anaingilia majukumu ya taasisi nyengine bila hata uoga? Kama kitenge anatamani usemaji wa club aende Azam kuwasaidia kuijenga fan base na huko ndiko kujemga ila kupambana na Haji manara kitenge asidhani hiyo vita atashinda kwani manara ni mwakilishi Simba Duniani ni timu yenye fan base kubwa wakiamua kumbomoa kitenge ni dakika tu licha ya kujitapa Kuwa ni mwandishi mkongwe. Sio kitenge tu mtu Kama Musa Mwakisu pale wasafi pia anamrengo wa chuki za dhahiri zidi ya Simba. Nadhani mwanahabari ni vyema kusimammia maadili ya kazi yake kuliko ushabiki. Na kwa kitenge kufurahia bato na Manara naona Kama vile mbwa aliejipeleka kwenye mdomo wa chatu hawezi kutoka Salama atakuwa tu Mashabiki wa Simba hawakumuacha khamisi kigwangala Salama.
DeleteWanaacha kuandika habari za uhakika kabisa za Mudadhir Abdallah kuchana nyavu akiwadungua Utopolo wanaandika habari za kichochezi ambazo hawana uhakika nazo.... Eti inasemekana, huna hakika acha uchochezi ..
ReplyDeleteAhahah hizo ni za uhakika kabisa wanakimbilia kwenye tetesi
DeleteWanataka kuwafurahisha akina matopolo ili kidogo wapate ahweni kutokana na maonevu wanayolalamikia ya kunyimwa ushindi
ReplyDeleteAndikeni na arusha mtu hana malinda
ReplyDeleteKitenge hana weledi inapohusu Yanga.Hajui afanye nini!Hana elimu ya journalism inayozuia kuwa partial kwenye reporting. Ethics za journalism zinakuzuia kuwa biased hata kama una interest na party mojawapo.
ReplyDeleteKitenge hata uchambuzi hajui
ReplyDeletekazi yake ujinga tu
ReplyDeleteKwann mnaaangaika na tetesi? Kama Kitenge Hana uweledi si muachanenae mnatumia nguvu kubwa ya nn?
ReplyDeleteKuzidi kumjibu ni kudhirisha kuna tatizo...!
duh
ReplyDeleteKwani Kitenge ni nani?
ReplyDelete