March 21, 2021


IMEELEZWA kuwa orodha ya makocha wanaowania nafasi ya kukinoa kikosi cha Yanga imefika patamu baada ya majina matano kupatikana kabla ya mchujo.

Vigezo ambavyo vimewekwa wazi na Yanga ni kwamba lazima kocha ambaye anakuja awe na mafanikio huko alikotoka pamoja na uwezo wa kuwapa mataji timu hiyo.

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa imekusanya pointi 50 baada ya kucheza mechi 23.

 Makocha ambao wanatajwa kuwa kwenye hesabu za kubeba mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7 ni pamoja na Hubert Velud pamoja na Sebastien Migne hawa ni Wafaransa na Mserbia Nikola Kavazovic.

Pia Etiene Ndayiragije raia wa Burundi ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania naye anatajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga.

Habari zimeeleza kuwa jina la Ndayiragije lilikatwa mapema baada ya wachambuzi wa CV kuweka wazi kuwa hatakuwa na mwendo mzuri ndani ya kikosi hicho.

Hiyo imetokana na falsafa zake ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania na hata alipokuwa ndani ya Azam FC pamoja na KMC bado alikuwa ni mzuri kwenye kujilinda kuliko kushambulia.


Pia jina la kocha wa Yanga wa zamani, Hans Pluijm nalo inaelezwa kuwa lipo kwenye orodha ya makocha wanaopigiwa hesabu na Yanga.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli aliweka wazi kwamba mchakato wa kupokea CV unaendelea na ukiwa tayari utawekwa wazi.


2 COMMENTS:

  1. PLUIJM AMEZEEKA TAYARI HATOWEZA PRESHA YA YANGA. MAANA HII YANGA NJAA TUPU

    ReplyDelete
  2. Nmecheka sn! Nmekumbuka kuna timu ilimleta kocha mzee kweli ht kutuliza mpira hawezi,,,,! Timu ikala za kutosha hd ikashuka daraja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic