RAIS mpya wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF Patrice Motsepe, bilionea wa Afrika Kusini na mmiliki wa Klabu ya Mamelodi Sundown amesema kuwa anapenda kuona soka la Afrika likipasua anga duniani.
Uchaguzi wake umefanyika leo Machi 11 nchini Morroco ambapo pia Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez alikuwepo pia.
Motsepe anachukua nafasi ya Ahmad Ahmad ambaye alikuwa mtangulizi wake na alikumbwa na skendo ya matumizi mabaya ya madaraka pamoja na matumizi mabaya ya fedha.
Uchaguzi wa leo ambao ulikuwa ni mkutano wa 43 wa Caf wapiga kura walikuwa na jina moja tu la mgombea ambaye ni Motsepe.
Akiwa na umri wa miaka 59 ni miongoni mwa matajiri na ameweka wazi kwamba anapenda kuona soka la Afrika likizidi kukua kila iitwapo leo.
"Soka la Afrika lazima likue na liwe bora duniani na haiwezi kuwa kwa usiku mmoja bali itatokea kwa muda na baada ya miaka kadhaa hivi karibuni itakuwa," .
0 COMMENTS:
Post a Comment