March 27, 2021

 


ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa Yanga, Patrick Sibomana amesema kuwa tayari amewasilisha malalamiko yake mbele ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kuhusu madai yake dhidi ya Yanga na kuambiwa jambo hilo linafanyiwa kazi na atapata majibu ndani ya miezi mitatu hadi minne.

 

Sibomana amekuwa katika mgogoro wa muda mrefu na waajiri wake hao wa zamani kutokana na kuwadai kiasi cha dola 4,000, sawa na shilingi milioni 9.2, ambazo zinatokana na fedha za usajili pamoja na sehemu ya mishahara yake.

 

Pande hizo mbili zimekuwa zikiwasiliana mara kwa mara ili kutafuta suluhu, ambapo nyota huyo aliwapa muda hadi kufikia Machi Mosi na kama wasingefanya, hivyo basi angepeleka malalamiko yake Fifa.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Sibomana alisema: “Ni kweli nimepeleka rasmi malalamiko yangu Fifa kuhusu madai yangu dhidi ya Klabu ya Yanga, hii ni baada ya kushindwa kuwa na muafaka mzuri kuhusu malipo ya fedha zangu, hivyo nimefikisha malalamiko yangu katika eneo ambalo naamini haki itatendeka.

 

“Fifa wameniambia kuwa suala hilo linafanyiwa kazi, na watanipa majibu ndani ya miezi mitatu hadi minne.”


Hivi karibuni kuhusu sakata hilo, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa aliliambia Gazeti la Championi: “Ni kweli tumepokea malalamiko ya Sibomana na tunaendelea kulifanyia kazi suala hilo," .

5 COMMENTS:

  1. Sasa tumekuwa wwadaiwa sugu na hili litawafanya waliopo hivi sasa kikosini wasiujuwe mustakbali wao na vipi turaraji morali katika nyoyo zao. Iliyobaki letu ni jicho tu tukiliona nyota likipepurishwa na upepo halijuwi litaangukia wapi

    ReplyDelete
  2. Saleh naona umesahau kuandika Sven Vandenbroeck nae ameishitaki Simba FIFA anadai Tsh Milioni 101 zinazotokana na bonus alizokuwa akiahidiwa

    ReplyDelete
  3. Wacha kujifariji. Sven ndio anadaiwa kwa kuvunja mkataba.Hixo tetesi zimeletwa na waandishi wa Utopolo kujifariji Umemsikia Sven akisema anaidai Simba??Bebeni mzigo wenu.

    ReplyDelete
  4. Sven kazungumza kwamba anadai??Yeye kavunja mkataba tena kwa kudanganya leo adai???Yeye ndio anadaiwa.

    ReplyDelete
  5. Lini mlisikia Mnyama kafikishwa fifa hasa katika ahadi ya Moooo kwa kesi za kudaiwa isipokuwa matopolo kwa kuitetea saini yao feki ya Morrison

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic