March 1, 2021


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, leo Machi Mosi kimeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania.

Mchezo huu wa leo ni wa 19 kwa Simba ikiwa ina mechi mbili mkononi ili kuweza kuwafikia vinara wa ligi ambao ni Yanga wakiwa wamecheza jumla ya mechi 21.

Mabao ya Simba yalifungwa na Chris Mugalu dakika ya 9 lile la pili lilifungwa na Luis Miquissone dakika ya 38 na kuwafanya mabingwa hao watetezi kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao hayo mawili.

Kipindi cha pili JKT Tanzania waliweza kuleta ushindani wakitaka kumtungua Beno Kakolanya ambaye alichukua nafasi ya Aishi Manula ambaye alipata majeraha na kupelekwa hospitali kwa huduma zaidi.

Licha ya jitihada hizo ngome ilikuwa ngumu kwa Simba chini ya Pascal Wawa aliyekuwa akifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Kenedy Juma, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na Tshabalala kwenye eneo la ulinzi.

Msumari wa tatu ulipachikwa na John Bocco dakika ya 90+3 kwa pasi ya Rarry Bwalya. 

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 45 kibindoni ikiwa nafasi ya pili huku vinara wakiwa na pointi 49.

5 COMMENTS:

  1. Ushindi muhimu japo rafu zilikuwa nyingi mno

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanapo cheza na timu kubwa mpira unaochezwa ni kama jihadi

      Delete
  2. Utopolo mtatusamehe, jengeni team kwanza wanaume wacha tuendele kufanya yetu

    ReplyDelete
  3. Watani wamo kutilia mkazo kwa Manara kutaka aombe Msamaha kwakuwa jezi haziuziki na wanataka walipwe pesa kuhusu Morrison na huku maendeleo ya timu kuwekwa upande lakini wanayataka makombe yote na ikionesha kama wamevunjika moyo harakati za zamani kimya. Watani nyanyukeni msikate chini Yanga ina tarehe kubwa sana kwani kudorora kwa Yanga ni kudorora kwa mpira nchini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic