April 26, 2021

 


ANDREW Simchimba jana Aprili 25 alikuwa nyota wa mchezo Uwanja wa Highlands, Mbeya wakati ubao ukisoma Ihefu 3-0 Coastal Union. 

Nyota huyo ambaye yupo Ihefu kwa mkopo akitokea Azam FC alitupia mabao mawili katika mchezo huo ambapo ilikuwa ni dakika ya 20 na 33.

Katika mchezo huo ambao ushindani ulikuwa ni mkubwa timu zote mbili zilionyesha uwezo wao huku Coastal Union wakishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata.

Msumari wa tatu ulipachikwa na mshambuliaji Raphael Daud ilikuwa dakika ya 36.

Mabao yote yalipachikwa kipindi cha kwanza jambo lililowafanya Coastal Union kuongeza nidhamu na kucheza kwa tahadhari kipindi cha pili huku wakipambana kusaka ushindi ila mambo yalikuwa magumu kwao.

Ushindi huo unaitoa Ihefu FC inayonolewa na Zubr Katwila nafasi ya 17 mpaka nafasi ya 13 baada ya kufikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 28.

Coastal Union inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda ipo nafasi ya 10 na pointi 33 imecheza jumla ya mechi 28.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic