WAKATI ishu ya mkataba wa beki wa kushoto, mzawa Mohamed Hussein, 'Tshabalala' likizidi kufukuta ndani ya Simba inaelezwa kuwa kuna nyota wengi ndani ya kikosi hicho ambao mikataba yao inatarajiwa kumeguka mwisho wa msimu huu.
Habari zinaeleza kuwa tayari mabosi wa Simba wameanza kufanya vikao ili kujua namna gani wanaweza kuwaongezea mikataba nyota hao ambao wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho.
Miongoni mwa nyota ambao mikataba yao ipo ukingoni ni pamoja na kiungo mkabaji, Jonas Mkude.
Kiungo mshambuliaji, Miraj Athuman.
Kiungo mkaabaji Mzamiru Yassin.
Beki mkongwe na kiraka ndani ya Simba, Erasto Nyoni.
Beki wa kati, Pascal Wawa.
Beki wa kushoto, Mohamed Hussein.
Kiungo mshambuliaji, Francis Kahata.
Mshambuliaji namba moja wa Simba Meddie Kagere mwenye mabao 11.
Nahodha wa Simba, mshambuliaji mzawa John Bocco mwenye mabao 10.
Beki Shomari Kapombe
Mume wetu Mo hawezi kuwaacha, atawaongeza mkataba ili watupe raha!
ReplyDeleteYeah utopolo chali ubingwa basi tena. Mpira sio fitina na maneno ya shombo mwisho wa siku shombo litakunisha mwenyewe.
DeleteUwepo wa Moo hapana atayeikimbia kwasababu hakuna dhulma wala ubabaushaj. Tazama wale wote waliokuwa matata kwengineko walitulia baada ya kufikia Simba na ndio mana Mpaka sasa hakuna panic ya kumramba miguu yeyote na hata mchezaji mwenyewe katulia kulinda pepo yake kwasababu ndege Mmoja mkononi ni bora kuliko wane msitu I na methali umesema KAMA HUNIJUI MIMI JARIBU MWENGINE.
ReplyDelete.