April 18, 2021

 




FT: Mwadui 0-1 Simba
Simba wanasepa na pointi tatu mbele ya Mwadui FC, Uwanja wa Kambarage na kuwafanya wafikishe jumla ya pointi 52 na Mwadui FC inabaki nafasi ya 18 na pointi 16.

Zimeongezwa dakika 4

Dakika ya 90 Mbisa anaanzisha mashambulizi kwenda kwa Manula
Dakika ya 85 Morrison anapiga shuti linakwenda nje ya lango
Dakika ya 83 Wawa anapeleka mashambulizi Mwadui
Dakika ya 79, Mzamiru anaingia anatoka Bwalya 
Dakika ya 71 Morrison anaonyeshwa kadi ya njano 
Dakika ya 67 beki wa Mwadui FC anaokoa hatari iliyopigwa na Kagere
Dakika ya 66 Morrison anapiga kona, inakutana na kichwa cha Onyango kinamaliziwa na Boco Gooool
Dakika ya 66, Chama anachezewa faulo nje kidogo ya 18, Wallace Kiango anaonyeshwa kadi ya njano 
Dakika ya 62 Chama anafanya jaribio linaokolewa na Mbisa
Dakika ya 59 Mbisa anaanzisha mashambulizi kwenda kwa Manula
Dakika ya 56 Bocco anaotea tena
Dakika ya 51 Bocco anaotea
Dakika ya 46 ametoka Chikwende kaingia Morrison, Mkude anaingia Bocco 
UWANJA wa Kambarage,  Shinyanga 
Mapumziko 
Zimeongezwa dakika 2
Dakika ya 45 Onyango anafinywa kiufundi na nyota wa Mwadui anafanya jaribio linakwenda nje ya lango 
Dakika ya 44 Bwalya anafanya jaribio inagonga mwamba 
Dakika ya 42 Kiango anapeleka mashambulizi Simba
Dakika ya 38 Chikwende anachezewa faulo
Dakika ya 37, Bwalya anafanya jaribio linakwenda nje kidogo ya lango 
Dakika ya 36, Chikwende anacheza faulo kwa nyota wa Mwadui FC 
Dakika ya 34, Chama anakosa nafasi ya wazi
Dakika ya 33, Chama anacheza faulo kwa nyota wa Mwadui
Dakika ya 31, Mbisa anaokoa faulo iliyopigwa na Bwalya
Dakika ya 29 Kagere anachezewa faulo 
Dakika ya 28, Simba wanapata kona ya tatu inaokolewa na Uhuru Seleman
Dakika ya 27,Chikwende anacheza faulo
Dakika ya 23 Bwalya anamwaga maji yanakwenda nje
Dakika ya 21 Mbise anaokoa hatari
Dakika ya 20, Mwadui wanapata kona haileti matunda 
Dakika ya 19 Uhuru anapeleka mashambulizi Simba
Dakika ya 15  Simba wanapeleka mashambulizi Mwadui
Dakika ya 12 Chikwende anaotea 
Dakika ya 11 Mbise anatoka kuokoa majalo anakosa na Simba nao wanakosa nafasi ya wazi
Dakika ya 10 mchezaji wa Mwadui FC anapewa huduma ya Kwanza 
Dakika ya 9, Chama anapoka mpira mikononi mwa Mbise, mwamuzi anaanua iwe faulo
Dakika ya 7 Zimbwe anarudisha pasi ya nyuma kwa Onyango 
Dakika ya 5, Chikwende anacheza faulo
Dakika ya 4, Chama anapiga kona ya Kwanza kwa Simba 

Dakika ya 2 Chama anafanya jaribio linaokolewa na Mbisa

Kipa wa Mwadui FC alipewa muda wa kubadili jezi kwa kuwa alivaa jezi inayofanana na Simba.

2 COMMENTS:

  1. Zimebaki mechi mbali ambazo Mfaransa alizitaka kutimiza mipango yake. Mabingwa walicheza kwa hadhari kubwa bila ya kutumia maguvu kujihifadhi kwakuwa mbele kuna akina Kaiza Chiefs. Pointi tatu kibindoni. Mnyama anatafuna muwa. Anaanzia upande wa kushoto na kumaliza wa kulia huku akisema simile kaa upande nipite

    ReplyDelete
  2. Case ya Morrison itaanza kuibuka Tena.Mchezaji wa Mwadui aliunawa mpira tukanyimwa penalt ya halali lakini cjackia Simba wakilalamika,ingekuwa Utopolo wangesema kesho tunajitoa kwenye league.Kweli nimeamini ukijua unajua tu.Mwaka huu watasusa Sana na Bado ,Simba hiyooooo semi final ya Caf club champion league

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic