April 19, 2021


 KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, 
amefunguka kwa sasa malengo yao ni kushinda mechi zilizobaki ili wajihakikishie nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao wameusotea kwa takribani misimu sita bila mafanikio.

Kwa sasa Azam FC inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 26.

Akizungumza na Spoti Xtra, Bahati raia wa Burundi, amesema: “Nafasi ya kupambania ubingwa bado tunayo, malengo yetu kwa msimu huu ni kupambana ili tuweze kuwa mabingwa na hili litafanikiwa endapo tutapambana kushinda mechi zetu zilizobaki.

“Kikubwa mashabiki wetu waendelee kutuamini, tunawaahidi mambo makubwa kwenye ligi na Kombe la FA.”

Ni mara moja tu Azam FC imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, ilikuwa msimu wa 2013/14.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic