April 19, 2021


 MSANII wa muziki wa Singeli kwenye ardhi ya Tanzania, Dulla Makabila amesema kuwa alikuwa ni shabiki wa Yanga kwa sababu familia yake aliikuta ikiwa upande huo jambo lililomfanya yeye pia awe shabiki wa timu hiyo.

Hivi karibuni Makabila aliomba kuwa shabiki wa timu ya Simba kwa kile alichoeleza kuwa ni maumivu aliyokuwa anayapata kutokana na matokeo ya timu hiyo aliyokuwa akiipenda awali.

Leo Aprili 19, Makabila ametambulishwa rasmi kuwa shabiki wa Simba na ameachia wimbo rasmi kwa ajili ya Simba. Unakuwa ni usajili mpya kwa upande mwingine kabisa ikiwa ni ule  wa mashabiki wa timu hiyo iliyo na tiketi ya kushiriki hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Makabila amesema:"Nilikuwa ninaipenda Yanga kwa kuwa niliikuta familia yangu ikiwa huko ila kutokana na maumivu ya matokeo ambayo yamekuwa yakipatikana nimeamua kuwa shabiki wa Simba kwa moyo wote,".

Haji Manara amesema kuwa Makabila atakuwa na jukumu la kuwa shabiki muaminifu wa Simba na atakuwa mtunzi wa nyimbo za Simba.

Wimbo wa leo amesema kuwa utatumika kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo:Wasafi

4 COMMENTS:

  1. Huyo sio mpenzi wa kweli wala shabiki wa kweli wa soka(ni shabiki maandazi).Shabiki wa kweli hata timu ikishuka daraja atashukanayo tu.
    Mashabiki dizaini ya Dulah Makabila hata ukimwambia akutajie first eleven ya timu yake hawezi kuijua,ukimuuliza timu yake imechukua ubingwa wa ligi mara ya mwisho lini hawezi kukuambia,timu yake ikiwa na mechi leo hawezi kujua pia.....so kwa dizaini hiyo ya mashabiki sishangai kusikia wamehama timu.
    All in all namtakia kila la heri ktk ushabiki wake kwa hiyo timu yake mpya.....ila ushauri wangu ni kwamba akiwa kule ajifunze nini maana ya ushabiki wa soka ili kesho tusije kusikia tena amehamia Namungo......ushabiki wa soka sio kama muziki,leo uko timu kiba kesho uko timu Mondi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shabiki uchwara... kesho wakianza kupigwa atasema toka mwanzo nilikuwa huku

      Delete
  2. Karibu Makabila kwenye Chama la ushindi.Mtaani kwangu Utopolo watatu washakuja Msimbazi.Simba oyeeeeee

    ReplyDelete
  3. Sio mtu wa mpira, anaangalia maslahi yake ya mziki, Yanga ikianzakufanya vzr atarudi, ndio itakua kinacho mpeleka ni maslahi zaidi, kama mtu ameanza kushabikia team kwasababu familia yake inashabikia basi hakua na maamuzi binafsi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic