April 13, 2021


MLINDA mlango namba moja wa kikosi cha klabu ya Azam, Mathias Kigonya ameshusha presha ya benchi la ufundi la klabu hiyo, baada ya ripoti za kitabibu kutolewa na kuonyesha kuwa majeraha ya nyota huyo ni madogo.

Kigonya alishindwa kumalizia mchezo wao wa Ijumaa iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kuumia bega la mkono wa kushoto, katika mchezo ambao Azam waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Raia huyo wa Uganda aliyekamilisha rasmi usajili wa kujiunga na Azam kwa mkataba wa miaka miwili Januari 14, mwaka huu akitokea klabu ya Forest Rangers ya Zambia, mpaka sasa ameichezea Azam mechi nane ambapo nne kati ya hizo hakuruhusu kufungwa bao yaani ‘Clean Sheet’.

Akizungumzia maendeleo ya kipa huyo Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Mlinda mlango wetu, Mathias Kigonya anaendelea vizuri na matibabu baada ya kupata majeraha madogo kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, ambapo kutokana na majeraha hayo alishindwa kuendelea na mchezo.

“Lakini tayari amepata matibabu na madaktari wetu wametuhakikishia kuwa anaendelea vizuri na ana nafasi kubwa ya kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo wetu ujao dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Aprili 16,”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic