April 13, 2021


MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa kesho Aprili 14 Uwanja wa Mkapa umefanyiwa mabadiliko ya muda na Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB).

Mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku ila taarifa rasmi iliyotolewa na TBLB umeeleza kuwa mchezo huo utachezwa kesho Aprili 14 saa 10:00 Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, ubao ulisoma Mtibwa Sugar 1-1 Simba.

Unatarajiwa kuwa mchezo mgumu kwa timu zote mbili kwa sababu Simba inapambana kutetea taji lake la ligi huku Mtibwa Sugar ikipambana kujinasua kwenye ligi.

Simba ipo nafasi ya tatu na ina pointi 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 20, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 15 ina pointi 24.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic