MWAKA mpya na mambo mapya ndani ya kikosi
cha Simba, mara baada ya kuliweka sokoni basi lao la timu ambalo
wamekuwa wakilitumia kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
Viongozi wa
Simba wameyasema hayo baada ya kusambaa picha mitandaoni zikionyesha
basi jipya likiwekwa stika zenye nembo za klabu hiyo.
Mtendaji
Mkuu wa Simba, Barabara Gonzalez aliliambia Championi Jumamosi kuwa,
wapo kwenye mpango wa kubadilisha basi hilo na kununua jipya, hivyo
wameliweka sokoni basi lao la sasa ili wapate fedha ya kuongezea gharama
za kununua basi jipya.
“Unajua hata ukitaka kununua simu mpya,
lazima uuze ile ya zamani kwanza, kisha uongeze hela za kununua hiyo
simu. Ndiyo tulichokifanya sisi tunataka kuliuza basi letu la zamani ili
tununue jipya,” alisema Barbara
Yote sawa tuu
ReplyDeleteSema hela hamna sifa tuu, kwan ukinunua jipya halafu ukauza lazamani si maumizi si yatapungua,
ReplyDeleteNaleo mnaenda kufungwa dadadeki!!!!
Hahaha dadadeki wapeleke wakopaji wenu 4g
Delete