IMEELEZWA kuwa uongozi wa Klabu ya Polisi Tanzania umewasimamisha nyota wao sita kutokana na tatizo la utovu wa nidhamu.
Taarifa imeeleza kuwa miongoni mwa nyota hao ni Rashid Juma ambaye yupo hapo kwa mkopo akitokea Klabu ya Simba aliomba ruhusa Februari 26 kuhudhuria harusi ya kakaye na alipewa siku tatu alipaswa kurejea Februari 29 hakufanya hivyo.
George Mpole, alipaswa kubaki kambini kwa sababu hakwenda kwenye mchezo dhidi ya Gwambina ila alitoroka kambini.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mpole na Rashid wamekuwa wakirudia mara kwa mara makosa hayo jambo ambalo limewafanya wawaambukize wachezaji wengine licha ya kupewa onyo wameshindwa kujirekebisha.
Wengine ni Pius Buswita, Tariq Seif, Abdulaziz Makame na Abdulmalick Adam.
Alipotafutwa Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro ili aweze kuzungumzia hilo hakuweza kupatikana.
0 COMMENTS:
Post a Comment