TOTTENHAM imemfuta kazi Jose Mourinho kutokana na timu hiyo kutokuwa na nafasi ya kushiriki Champions League msimu huu.
Mourinho, mwenye miaka 58, alichukua mikoba ya Mauricio Pochettino Novemba 2019 ila mwendo wake umekuwa tofauti na wengi walivyotarajia baada ya kufeli kwenye Europa League.
Ni siku sita zimebaki kabla ya Tottenham kukutana na Manchester City kwenye mchezo wa fainali ya Carabao. Uwanja wa Wembley.
Inatajwa kuwa Ryan Mason na Chris Powell wanapewa nafasi ya kuifundisha timu hiyo kabla ya msimu huu kukamilika.
Kocha huyo wa zamani wa Klabu ya Manchester United, Real Madrid mchezo wake wa mwisho ilikuwa ni dhidi ya Everton na ubao ulisoma mabao 2-2.
Nilijua tu kuwa baada ya kumvunjia heshima Mauricio Pochetino na kumchukua huyu jamaa anguko la Tottenham lilikuwa limewadia.Mourinho sio kocha kabisa huwa anabebwa na uwezo binafsi wa wachezaji hasa katika zile timu zenye kutumia fedha nyingi kusajili wachezaji bora wa gharama lakini sio kwa timu kama Tottenham ambayo haina uwezo wa kurundika wachezaji bora kutoka timu nyingine
ReplyDelete