April 19, 2021


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier 
Gomes, amefunguka kwamba, msimu huu anataka kurudia mafanikio yake ya kufika nusu fainali kwenye michuano inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).


Kocha huyo raia wa Ufaransa, ameongeza kwamba, anataka kurudia rekodi hiyo ya mafanikio makubwa ambayo aliiweka akiwa anainoa Cotton Sports ya Cameroon walipofika nusu fainali katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Msimu huu, Gomes ameiongoza Simba kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakimaliza kileleni mwa msimamo wa Kundi A kwa kukusanya pointi 13.

Kocha huyo mwaka 2014 aliifanikisha Cotton Sports kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo walitolewa na Al Ahly.


“Tulicheza nusu fainali nikiwa na Cotton Sports kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mbele ya Al Alhy, lakini tukapoteza, nina matumaini makubwa ya kufika mbali na kikosi ambacho ninacho kwa sasa.

“Bado kazi inaendelea, tunatakiwa kupambana zaidi kuliko ilivyokuwa miezi mitatu iliyopita na kikubwa tunatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa sababu michezo inayokuja ni hatari sana,” aliweka nukta kocha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic