April 13, 2021


 MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Abdulazack kwa sasa muda wake wa kuishi Bongo upo ukingoni baada ya mkataba wake wa miezi sita kuwa kwenye hatua za mwisho kukamilika.

Raia huyo wa Burundi alisaini dili la miezi sita na pale msimu utakapokwisha naye inaelezwa kuwa atapewa mkono wa kwa heri.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa nyota huyo zimeeleza kuwa tayari ameshaambiwa kwamba hataongezewa mkataba kwa kuwa bado hajaonyesha yale makali ambayo alikuwa nayo.

"Fiston kwa sasa muda wake umeisha na anajua kwamba hataongezewa mkataba kwani kazi ambayo alikuwa amepewa inaonekana bado haijaeleweka," ilieleza taarifa hiyo.

Raia huyo wa Burundi ndani ya ligi amefunga bao moja ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania wakati wakigawana pointi mojamoja na ana bao moja kwenye Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora ilikuwa dhidi ya Ken Gold.

Hivi karibuni Fiston alisema kuwa anatambua uwezo wake na alisaini dili la miezi sita kwa kuwa hajawahi kudumu na timu kwa muda mrefu kutokana na ofa ambazo huwa anapata.

"Sijawahi kuwa kwenye timu moja kwa muda mrefu kwa sababu huwa ninakuwa na ofa nyingi sina tatizo na uwezo wangu,".

4 COMMENTS:

  1. Sasa ukimwambia mchezaji hivyo unategemea morale ya kupambania timu itakuwepo?Acheze kwa nguvu aumie???

    ReplyDelete
  2. Goli lenyewe alilofunga alikuwa kwenye offside position ����

    ReplyDelete
  3. Timu imrpoteža utulivu wakati ambao wanautaka ubingwa. Huyu ndani huyu nje. Ni kweli kabisa kwakuambiwa mbele kuwa hatobaki na mchezaji bado yumo ndani ya nini unararaji. Nakumbuka mchezaji huyo alipata upokeži usio na mfano hapo Airport na leo anaambiwa hafai

    ReplyDelete
  4. Yanga inakosa welekeo
    Kwa kuwa na kamati mbovu ya usajili Lakini pia wanasajili wachezaji YouTube hili ni tatizo wachezaji wanapewa mikataba bila inteveu Hii ni hatar tupu yani
    Hatuwez kupiga hatua

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic