April 26, 2021


 KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Didier 
Gomes amegoma kuona mastaa wake wakiondoka kwenye kikosi chake katika msimu ujao.


Kati ya mastaa wanaotajwa kuondoka Simba ni Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ anayedaiwa kusaini mkataba wa awali Yanga, Joash Onyango kwenda Orlando Pirates na Aishi Manula kuwaniwa na Mamelodi Sundowns zote za Afrika Kusini.


Zimbe Jr au Tshabalala hivi sasa  anaelekea kuwa mchezaji huru kwa kuwa mkataba wake unaelekea mwishoni.

“Muda wa usajili bado lakini nimeona vema

kulizungumzia hili la wachezaji wangu

wanaodaiwa kuondoka Simba mwishoni

mwa msimu huu baada ya mikataba yao

kumalizika.


“Binafsi sitakubali kuona wachezaji wangu hao wakiondoka kutokana na umuhimu mkubwa waliokuwa nao katika timu, kwani siku zote ni hatari kwa timu kufanya mabadiliko ya kikosi kwa kuwaondoa wachezaji walioipa mafanikio timu hasa msimu huu kimataifa.


“Lakini kingine sifahamu kuhusu kuondoka

kwao, kitu kikubwa nitakachoweza kusema

kuwa natamani kubakia na wote katika

misimu mingine miwili hadi mitatu katika

kutengeneza timu bora kwa ajili ya

mafanikio ya timu, ” alisema Gomes.

Chanzo:Championi

5 COMMENTS:

  1. Kama ni kweli Tashabala anataka kujiunga na Yanga, kwanza ajiulize kwanini wale mastaa wakubwa waliojiunga na Yanga baada ya kufikia huko tu ule uwezo wao ulipotea mojakwamoja na kubskia wakizomewa na mashabiki. Kwahivo tunakuhsdhirisha jiti na macho baba. Usiwache chako kwa msala upitao. Usiwache waliokuwa ukafika hapo ulipo. Ujuwe nyota yako ipo kwa Simba na hapo kwengine katu

    ReplyDelete
  2. Wewe si ndio ulituletea habari za Chama kusaini yanga au unatuona kama wale wa upande wa pili ambao walidanganywa Morison kafunguliwa kesi cas

    ReplyDelete
  3. Zimwe kasaini mkataba wa awali utopolo? Hizo ni mind games za yanga, hawana uba u huo na yeye atakuwa hana kichwa

    ReplyDelete
  4. SASA utatokaje kwenye tiny bora ukaenda kwenye timu mbovu kama yanga , wenzake wanaenda sauzi yeye anaenda utoporo fc siundezi huo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic