MANCHESTER City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola jana ilitwaa taji la nne la Carabao Cup mfululizo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur, Uwanja wa Wembley.
Bao la ushindi lilifungwa na beki Aymeric Laporte dakika ya 82 kwa pasi ya Kevin de Bruyne mbele ya mashabiki 8,000 ambao waliruhusiwa kwa kuwa bado tahadhari ya Corona inachukuliwa.
City imefanikiwa kutwaa taji hilo kuanzia 2018 hadi 2021 jambo ambalo ni mafanikio makubwa kwa timu hiyo inayopewa nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu England.
Baada ya mchezo huo nyota wa kikosi cha Spurs, Son HeungMin alionekana akitokwa na machozi na kufarijiwa na wachezaji wa City.
Guardiola amesema kuwa anawapongeza wachezaji wake kwa kufanya vizuri na kutwaa taji hilo muhimu.
0 COMMENTS:
Post a Comment