April 26, 2021

 HARUNA Niyonzima,  kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa bado wana nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa wana mechi nyingi mkononi.



Jana, Aprili 25, ikiwa Uwanja wa Mkapa ilishuhudia inayeyusha pointi tatu jumlajumla kwa ubao kusoma Yanga 0-1 Azam FC. 


Bao pekee la ushindi la Azam FC lilifungwa na Prince Dube ambaye ana mabao 12 akiwa ni kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara. 


Niyonzima ambaye alianzia benchi alipata muda wa kuonyesha makeke yake kipindi cha pili ila jitihada zake hazikuleta matunda na kuacha pointi tatu kwenda Azam FC. 


Nyota huyo amesema:" Mchezo ulikuwa mzuri na ni makosa ambayo tunayafanya wapinzani wetu wametumia kutufunga.

"Jambo la msingi tushikamane na sasa ubingwa bado tuna mechi nyingi,".

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 27 imekusanya pointi 57 ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ina mechi 7 mkononi.

7 COMMENTS:

  1. Daaah!! Hiyo bhange mnayo vuta siyo ya Dunia hii, pengine imetoka sayari ya Mars!!! Ubingwa upi tena labda mna mpango wa kuiba kombe la ligi kuu. Viongozi + wachezaji + mashabiki = wote mna imani ya kuchukua ubingwa!!! Hakika mmerogwa nyie!!!.

    ReplyDelete
  2. Masikini roho yake. Wenye Yanga tayari wameshanyanyuwa mikononjuu. Huna budi kuchunga kibaruwa chako

    ReplyDelete
  3. Wameshachukua mapinduzi ndo size yao.. Acheni kuzuga hebu tuandikieni habari za dube

    ReplyDelete
  4. Kwan Dube anasemaje kuhusu like goli la kikatili

    ReplyDelete
  5. Vipi itashinda Yanga wakati utawasikia mashabiki badala ya kushajiisha timu wamekuwa wakiwakashifu viongozi toka juu Mpaka chini kwa lugha ambayo muungwana yoyote inasikitisha kuisikia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic