April 6, 2021

 

 


ALIYEWAHI kuwa nyota wa klabu ya soka ya Yanga na timu ya Taifa , Taifa Stars Ally Mayay amesema kuwa uwezo mkubwa wanaouonyesha wachezaji Clatous Chama na Luis Miquissone katika kufunga na kutengeneza mabao ni miongoni mwa sababu kubwa zinazoibeba Simba.

Miquissone na Chama wamekuwa katika kiwango cha hali ya juu msimu huu ambapo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika nyota hao wawili wamehusika katika mabao 13 katika michezo tisa waliyocheza.

Chama amefunga mabao manne na kuasisti mara tatu, huku Miquissone yeye akifunga mabao matatu, kaasisti mabao mawili na kutengeneza penalti moja.

Kutokana na uwezo mkubwa wanaouonyesha, nyota hao wawili walichaguliwa kuwa katika kikosi bora cha wiki cha Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumzia ubora wa nyota hao, Ally Mayay kuhusu uwezo wa nyota hao amesema: “Ni suala lililowazi kwamba Simba kwa sasa wapo katika kiwango bora kabisa, na hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa na kuendana kwa falsafa ya timu hiyo na aina ya wachezaji walionao.

“Falsafa ya Simba kwa miaka yote ni kucheza soka la kumiliki mpira na nadhani kwa sasa wamefanikiwa zaidi katika hilo kwa kuwa wana wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kama ilivyo kwa Luis na Chama,”

Licha ya kuwa na mchezo mmoja mkononi Simba tayari imefuzu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, baada ya kujikusanyia pointi 13 katika michezo mitano waliyocheza mpaka sasa.

 

4 COMMENTS:

  1. Nyambaf!!!!! Aliyeongea ni mtu binafsi na katoa maoni yake kama mtu binafsi lakini vilaza wa Saleh Jembe kama kawaida yao wanatundika kichwa cha habari YANGA

    ReplyDelete
  2. Waropokaji wapo wengi tu utopolo

    ReplyDelete
  3. Simba chama kubwa, asiye na akili ndiye anayepinga

    ReplyDelete
  4. Ata kama yaan kichwa cha habar na habar yenyewe haviendan yaan hawa wandsh ni vchekesho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic