April 20, 2021


 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wanatambua kwamba Simba ni timu imara watawaheshimu kwenye mchezo wao wa kesho na wataingia uwanjani kwa hesabu za kusaka pointi tatu muhimu.

Baraza anatambua aina ya wachezaji wa Simba kwa sababu msimu huu alikutana nao zama zile alipokuwa ndani ya Biashara United na kesho anakutana nayo akiwa na Kagera Sugar.

Ukitazama msimamo, Kagera Sugar imejijengea ngome yake nafasi ya 14 imekusanya pointi 27 baada ya kucheza mechi 26 wapinzani wao Simba wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 52 baada ya kucheza mechi 22.

Baraza amesema:"Ipo wazi kwamba Simba ni timu imara ila haina maana kwamba tunawahofia, tunaamini kwamba baada ya dakika 90 tutakuwa na kitu ambacho tutakipata.

"Kikubwa ni wachezaji kufuata yale maelekezo ambayo nimewapa na maandalizi yapo kamili hivyo mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," amesema.

 Mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa kwa sababu, Kagera Sugar inapambana kubaki ndani ya ligi wakati Simba inapambana kuweza kutwaa taji la ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic