AMEFUNGAAA ilikuwa ni sauti ya mtangazaji wa Azam TV, Pascal Kabombe wakati akitangaza bao la mfungaji wa kwanza kwa bao la Yanga, Ditram Nchimbi ambaye alifunga bao hilo akiwa nje ya 18 kwa pasi ya Deus Kaseke.
Wakati ubao ukisoma Yanga 3-1 Gwambina kwa Yanga, Nchimbi alianza kupachika bao la kuongza dakika ya 18 kisha bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili ambapo Gwambina iliweza kuweka usawa kupitia kwa Jimsone Mwanuke, dakika ya 49.
Hawakuwa wanyonge Yanga dakika ya 52 beki Bakari Mwanyeto alipachika bao la pili na lile la mwisho lilipachikwa na Saido Ntibanzokiza ambaye alichukua nafasi ya Tuisila Kisinda aliyeumia kipindi cha pili.
Baada ya kupachika bao hilo Saido alionekana akiomba kufanyiwa mabadiliko kisha alitoka nje ya uwanja kabla ya Juma Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga kuonekana akiongea naye ili kumrejesha uwanjani.
Licha ya Gwambina kupoteza kwa kufungwa leo walicheza soka la darasani wakiwa wametulia hivyo wakiendelea na aina ya mpira ambao wamecheza leo Uwanja wa Mkapa kutakuwa na ushindani mkubwa katika mechi zote za ligi.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuzidi kuwa namba moja kwa kuwa inafikisha jumla ya pointi 57 baada ya kucheza mechi 26 huku Gwambina ikibaki na pointi 30 ipo nafasi ya 12 na pointi 30.
0 COMMENTS:
Post a Comment