April 14, 2021

KIUNGO wa zamani wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Ally Mayay amesema kuwa kama Simba wataendelea kuwa na nidhamu kubwa ya kucheza ugenini na kuwekeza katika mbinu za kutafuta matokeo, basi kwa ubora wa kikosi chao ana matumaini makubwa klabu hiyo itatinga hatua ya nusu fainali.

Simba imefuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuongoza kundi A la michuano hiyo kwa kukusanya pointi 13 katika michezo yao sita waliyocheza.

Simba sasa wanasubiri kupangwa dhidi ya klabu moja kati ya CR Belouizdad, USM Alger zote za Algeria au Kaizer Chief ya Afrika Kusini kwenye michezo ya robo fainali katika droo itakayopangwa Aprili 30, mwaka huu.

Akizungumzia kiwango cha Simba Mayay amesema: “Ni jambo lililowazi kuwa kama utazungumzia kiwango cha wakati huu basi Simba ni miongoni mwa timu bora Afrika, kumaliza kama vinara wa kundi lao ambalo yumo bingwa mtetezi (Al Ahly) ni miongoni mwa mambo ambayo yanathibitisha hilo.

“Silaha kubwa ya Simba msimu huu imekuwa katika umiliki wa mpira na wamefanikiwa sana hapo, lakini wanapoenda katika hatua ya robo fainali wanapaswa kutambua kuwa, hiyo ni michezo ya mtoano ambayo jambo la muhimu zaidi ni kupata matokeo na si kingine.

“Hivyo, wanapaswa kuhakikisha wanaweka nguvu kubwa ya kucheza kwa nidhamu hasa katika uwanja wa ugenini ili kuhakikisha kuwa hawaruhusu bao au kupunguza idadi ya mabao ya kufungwa, lakini pia wanapaswa kutumia vizuri faida ya kucheza nyumbani kwa kupata matokeo kama ambavyo wamekuwa wakifanya, naamini Simba watafuzu nusu fainali,”


1 COMMENTS:

  1. Uwa napenda uchambuzi wa Ally Mayay. Atakichambua mchezo wa Yanga na Simba uwa anausema uhalisia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic