MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo Aprili 14 wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa, Uwanja wa Mkapa.
Chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes Simba ilifanikiwa kupachika bao la kwanza dakika ya 9 kupitia kwa Clatous Chama.
Alikuwa ni Luis Miquissone ambaye alichezewa faulo kisha jukumu la kupiga faulo hiyo akapewa Chama aliyefunga bao hilo la kwanza akiwa nje ya 18.
Bao la pili lilipachikwa na Rarry Bwalya dakika ya 19 na bao la tatu lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 43 na kuwafanya Simba kuenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa 3-0.
Kipindi cha pili Simba waliongeza mabao mawili kupitia kwa Kagere dk 51 na Luis Miquissone dakika ya 73.
Simba wanasepa jumla ya pointi nne kwa Mtibwa Sugar kwa kuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Jamhuri,Morogoro ubao ulisoma Mtibwa Sugar 1-1 Simba.
Inafikisha pointi 49 ikiwa ipo nafasi ya pili huku Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya 15 na pointi 24 baada ya kucheza mechi 24.
Utopolo wakiona Mambo haya ndo wanachanganyikiwa kabisa
ReplyDeleteEti wanalalamika kuwa Mnyama amependelewa na wanajiandaa kwenda tff kushitaki
DeleteWana Yanga tunawatangazia maandamano ya amani kesho kushinikiza TFF wawaambie wapunguze kupiga pasi nyingi na kuwafunga wapinzani wao goli nyingi-tunaamini TFF ni wasikivu watashughulikia suala hili
ReplyDeleteSimba hii inabidi ipunguze sifa maana vipigo vya 5G utaanza kusikia tusipopewa penalt tunajitoa kwenye league,case ya Morrison nayo itaibuka upya kesho,mara marefa wafungiwe kwa kusababisha watu wapigwe 5G,wanasahau As Vita naye alikula 4G sijuia naye atashitaki caf Simba wamewabambikia Corona.Kwa kifupi ni kwamba Utopolo huu muziki hawauwezi hata kidogo,wajipange mwakani ila wakiendelea kufukuza makocha 5G inawahusu
ReplyDeleteVipi wadau nauliza kituo kinachofuata ni .......
ReplyDeleteshinyanga kuifuata Mwadui. Mechi ni Jumapili tarehe 18.04
DeleteAhsante mdau kwa taarifa
Delete