April 1, 2021

 


UONGOZI wa Klabu ya KMC umesema kuwa umeanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.


Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi Aprili 8 baada ya kusimama kwa muda kutokana na maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya tano, John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17,2021.

Tayari Bodi ya Ligi Kuu Bara, (TBLB), imetoa ratiba iliyofanyiwa marekebisho ambapo mchezo wa kwanza ligi itakapoendelea baada ya kusimama, KMC itakutana na vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga.

Yanga ipo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 50 baada ya kucheza mechi 23 itawakaribisha KMC walio nafasi ya tano na pointi 35 baada ya kucheza mechi  24.

Chritina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema:"Wachezaji wa Klabu ya KMC FC, tayari wameanza kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga mchezo utakaopigwa Aprili 10 katika Uwanja wa Mkapa, Jijini Dar es Salaam saa 1:00 usiku,".


Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa CCM Kirumba,  ubao ulisoma KMC 1-2 Yanga hivyo utakuwa ni mchezo wa ushindani kwa timu zote mbili.

KMC watapambana kulipa kisasi huku Yanga wakihitaji kulinda rekodi yao ya kusepa na pointi tatu mbele ya KMC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic