WAKATI uliopo kwa sasa kwa timu zote ambazo zinashiriki Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza pamoja na Ligi ya Wanawake Tanzania ni kupiga hesabu za mwendo wao ambao wanakwenda nao.
Ukitazama kwa haraka kila timu inapoanza
msimu imekuwa ikiweka malengo ila mwisho wa siku inakuwa ngumu kuona kama
yametimia au la kwa kuwa hawana muda wa kuyatazama.
Ikiwa timu zitapata muda wa kujipanga upya
itakuwa kazi rahisi kwa kila mmoja kufurahia mafanikio ambayo watayapata.
Kupitia mchakato wa kutazama kule ambako
timu imetoka na ilipo inatoa taswira kamili ya kupata kile ambacho timu
inahitaji kuwa nacho wakati ujao.
Kwa kufanya hivyo itatoa fursa ya timu
kujua pale ambapo imekosea na kuanza upya pale ligi itakaporejea kwa kasi kwa
kuwa mzunguko wa pili kila timu inapambana.
Tunapitia kwenye kipindi kigumu kwa sasa,
ipo wazi ila ni somo kwamba hapa dunia kwetu ni njia na kila mmoja lazima
ajiandae kwa ajili ya jambo hilo.
Kwa familia ya michezo imeona namna ambavyo
kuondoka kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli
ametuacha Watanzania kwenye majonzi.
Muda ambao timu zitakuwa zinatafakari
kuhusu kuanza maisha mapya bila uwepo wake ni muhimu pia kutazama yale ambayo
yalikuwa yamepangwa kufanywa na timu husika.
Kupenda kwake michezo kulikuwa wazi kwa
kila Mtanzania na wapenda michezo kwa kuwa alikuwa anajitoa na kutumia muda
wake zama za uhai wake kuzungumza na wanamichezo.
Ni ngumu kwa timu kufikia malengo ambayo
alikuwa anafikiria shujaa wetu Magufuli kwa kuwa yalikuwa ni maono makubwa ila
lazima yafikiriwe kwa kila timu.
Ndoto yake kubwa ilikuwa siku moja aone
timu ya Tanzania ilete ubingwa wa Afrika jambo ambalo halikukamilika mpaka
anaondoka hivyo ni muhimu kila timu kupiga hesabu za pale ambapo zilikwama.
Ni Muda wa maandalizi unatumika kurekebisha makosa ambayo yanafanywa ndani ya uwanja. Kila mchezaji anajukumu la kufanya kazi yake kutimiza majukumu anayopewa.
Maandalizi ni muda huu na sio wakati wa
kucheza mechi za ushindani. Muda ule huwa unakuwa maalumu kuweza kuona kile
ambacho walikuwa wakifanya mazoezi.
Matokeo yanatafutwa kwa kila mmoja kufanya
vizuri kuanzia kwenye maandalizi kabla ya mchezo wa ushindani.
Jambo kubwa la kufanya ni kukubali
kujifunza na pale ambapo mnakosea mna kazi ya kurekebishana wenyewe kwa wenyewe
ili kusaka matokeo kwenye mechi zenu ambazo mtacheza.
Kila mchezaji anapenda kuona timu inapata
matokeo mazuri. Ikiwa morali itakuwa kubwa kwa kila mchezaji itaongeza nguvu
pia ya kupata matokeo mazuri wakati ujao kwenye mechi za ushindani.
Imani yangu ni kwamba kila kitu
kinawezekana. Ili kuweza kujiondoa kwenye ile presha ya kushuka daraja ama
kukosa ubingwa ni muhimu kila mmoja kutimiza majukumu yake bila kusukumwa.
Zipo timu ambazo zinaiwakilisha Tanzania
kwenye mashindano ya kimataifa nazo zina kazi ya kuweza kufanya vizuri na
kutazama pale ambapo zilikuwa zimekosea awali.
Namungo FC ilikwama kwenye mechi zake zote
mbili za kimataifa katika Kombe la Shirikisho, ile ya ugenini na nyumbani. Hakuna
haja ya kukata tamaa muhimu kuangalia pale ambapo timu ilikosea.
Ikiwa wachezaji watakata tamaa muda huu
wakati wa kupata matokeo chanya itakuwa ngumu kwa timu hiyo kushinda kwa sababu
hakutakuwa na nguvu ya timu hizo kusaka ushindi.
Yote kwa yote ni jukumu letu kufanya yote
kwa juhudi ili kupata matokeo mazuri ambayo ni furaha kwa mashabiki.
Na namna ambavyo timu itakuwa inapata
matokeo itakuwa ni furaha pia kwa Watanzania wapenda michezo.
Simba ambayo inawakilisha nchi kwenye Ligi
ya Mabingwa Afrika ikumbuke kuwa ina kazi ya kusaka ubingwa wa Afrika na
inawezekana ikiwa kutakuwa na mipango makini.
Kuongoza kundi haina maana kwamba imemaliza
kazi hapana inajukumu la kusaka ushindi kwenye mechi zake zizilizobaki ili
kufikia malengo.
0 COMMENTS:
Post a Comment