April 7, 2021


 WAKATI wakiwa kwenye harakati za kukwea pipa jana kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, mabegi ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez yalimvunja mbavu aliyekuwa Mtendaji wa Simba, Crescentius Magori.

 

Barbara aliripoti Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa 7:45 mchana na kupokelewa na Magori ambaye alianza kwa kucheka.


Magori alikuwa akitazama mzigo aliokuwa amebeba Barbara ambao ulikuwa na mabegi manne, matatu makubwa na moja lilikuwa dogo.




Magori alisikika akisema kuwa:- “Hahaha mabegi yote hayo uliyobeba hakika una jambo lako.”


Simba kwa sasa imeshatia timu nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 9, Uwanja wa taifa wa Cairo ambapo mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 1-0 Al Ahly.

3 COMMENTS:

  1. Safari za akina mama huwa balaa

    ReplyDelete
  2. Mwanamme hutoa ufunguo mfukoni hatuwa ishirini kabla hajafika mlango I lakini mwanamke huabza kuutafuta ufunguo pale anapofika mlango I na huku akilalamikia "jamani mbona siuoni ufunguo" ndio walivo dada zetu

    ReplyDelete
  3. Sasa apo topki ni nini jaman mbna cja elewa?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic