April 7, 2021


 SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) limefafanua kuwa adhabu aliyopewa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kuwa imeegemea kwenye upande wake wa uongozi wa klabu na si kwenye masuala mengine ya kama vile kumzuia asifuatilie taarifa za michezo.

 

 Ndimbo amejibia malalamiko ya Makamu Mwenyekiti huyo aliyefungiwa kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 5 na faini ya shilingi milioni 7 kuwa, siku tatu zilizopita alisema amezuiwa asisome magazeti ya michezo wala kutazama runinga.

 

 Ndimbo amesema;- “Kama ambavyo taarifa ya adhabu ilivyosema na ni tofauti na alivyoielezea kwamba haruhusiwi hata kusoma magazeti au ikifika kwenye taarifa za michezo azime TV asiangalie. 


"Adhabu aliyopewa ni kwamba majukumu yake ambayo amekuwa nayo ndipo aadhabu ilipoegemea.

 

 

“Asijihusishe na majukumu hayo ya kiuongozi kwa muda huo ila mengine kuhusu kutokusoma magazeti labda alikuwa anafurahisha genge tu.”

 

 

(Aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela ambaye kwa sasa amefungiwa miaka 5).

 

 

Ndimbo amesema Mwakalebela amefungiwa kimajukumu ya Uongozi lakini ana nafasi ya kushuhudia michezo viwanjani kama mashabiki wengine.

 

 

“Linapokuja suala la kwenda uwanjani hilo sio kujishugulisha na suala la uongozi wa mpira na maana yake umekwenda kama mtazamaji mwingine.”

13 COMMENTS:

  1. Alitaka tuu kuwadanganya wale wasiotumia akili ila werevu tulijua hiyo ni chai ya mchana tuu.

    ReplyDelete
  2. Hivi hili jamaa kuna wakati linasema ukweli?Kila siku uongo tu na kuzusha.

    ReplyDelete
  3. Zee zima hovyoo! Mpaka aiponza utopolo na bila shaka huyu ndo muasisi wa sababu yakuitwa utopolo klabu anajiropokea tu

    ReplyDelete
  4. Yanamwisho hayo hata rage alipokuwa fat alikuwa mungu MTU lakini zama zake zilishapita

    ReplyDelete
  5. Malinzi yeye alikuwa nani

    ReplyDelete
  6. Kumfungia miala mitano na faini milioni 7 hayo ni maamuzi ya kipuuzi ni si kiuana michezo, hasa kwa kuzingatia kosa lenyewe kuna mijiti iliibia hiuo TFF mamilioni na kudhoogisha soka wala hawajawai kukutana adhabu kubwa kiasi hicho. Michezo ni urafiki ,afya na burudani siyo kukamiama na kukomoana kutokana na usimba na uyanga ni mambo ya ajabu sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Adhabu zote zinazotolewa zipo kwa mujibu wa kanuni kutokana na uzito wa kosa na wala sio kumkomoa mtu. Huyo nyamtumbo aliambiwa athibitishe madai yake akashindwa kwa maana hiyo alisema uongo ili tff ionekane kweli imeshapanga bingwa wa ligi. Nadhani miaka mitano ni michache wangempa cha maisha

      Delete
  7. Walijiona wababe wa kuogopwa na hayo ndio matokeo ya ubabe wao kwa kila pahala yakiwemo yale ya kupiga na kuwachania nguo wasioutaka ugomvi. Tuzitunze kauli zetu kwasababu ni afadhali kujikwaa kidole kuliko kujikwaa ulimi, ubabe usio na mingi ni kama ule walipompa Haji Manara wiki mbili awatake radhi eti alitumia lugha iliyopelekea kutouxika jezi zao. Jee Manaara aliyatmiza hayo na nini walichokifanya dhidi yake? Kimyaaaa

    ReplyDelete
  8. Mpumbavu huyu jamaa. Hana akili kabisa

    ReplyDelete
  9. Hata hivyo tff imemchewesha kumpa adhabu

    ReplyDelete
  10. Tff kiongozi tumchague sisi wanayanga arafu nyie mmufungie.haya endelezeni umungu MTU hapo ofisi kumbukeni zama za rage pale fat.kiama chenu chaja

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dua ya kuku haimpati mwewe...huyo kafungiwa mitano lkn Karia mitano tena TFF....Povu ruksa.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic