UONGOZI wa Yanga umesema kuwa licha ya kupoteza mchezo wao jana mbele ya Azam FC bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zijazo na hawajakata tamaa.
Uwanja wa Mkapa, saa 2:15 usiku, kulikuwa na mpambano mkali kwenye mchezo wa ligi ambapo Azam FC ilishinda bao 1-0.
Ni Prince Dube ambaye alipachika bao pekee la ushindi dakika ya 85 kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango, Faroukh Shikalo na kuwafanya wapoteze mchezo huo wa mzunguko wa pili.
Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga amesema kuwa ni matokeo mabaya ambayo wanayapata watayafanyia kazi.
"Hakuna kukata tamaa. Tuendelee kupambana kwenye kila mchezo kwa kila namna ibakie matokeo ya mpira na bahati ya siku yenyewe."
Azam FC inafikisha jumla ya pointi 54 ikiwa nafasi ya tatu huku Yanga ikibaki kuwa na pointi 57 nafasi ya pili kwenye msimamo. Kinara ni Simba mwenye pointi 58 baada ya kucheza mechi 24.
Jitoeni kwenye ligi,pumbavu zenu mnaongea sana utopolo,kukaa siti ya mbele haina maana kwamba wewe unalipa nauli kubwa,Safari ni moja tu na nauli ni ileile punguzeni majigambo na huyo kocha wenu hamalizi mechi za msimu anafukuzwa.
ReplyDeleteDuh sasa sie Utopolo tunafanyaje maana ubingwa ndio umeshatukimbia...tuandamane Kwa waziri na TFF kuwa Prince Dube hana adabu kwa mshuti ule uliomfanya Shikalo kulia usiku mzima
DeleteMsemaji wa uto alijigamba kuwa tar 25 ni send-off kumbe wanachukuliwa jumla
ReplyDeleteIli kufanikiwa katika jambo lolote unatakiwa kukamilika katika mambo 3 tu.
ReplyDelete1. Afya ya akili
2. Afya ya kimwili
3. Afya ya kiroho
Yanga ina athiriwa na mambo hayo matatu kutokukamilika ipasavyo, kuanzia kwa uongozi, wachezaji na mashabiki.
Uongozi una sajili wachezaji wabovu magarasa wasiokuwa na timu ama majeruhi au walioachwa na timu zao huko walikotoka, mchezaji huru " free agent" ambaye unamchukua ili kukwepa gharama za kuvunja mikataba, una sajili " cheap or free players" ukitegemea watakupa ubingwa kwenye ligi yenye ushindani kama ya Tanzania, ligi ambayo lazima uwe na wachezaji imara na wenye vipaji na pia uwe na nguvu ya pesa kuwanunua waamuzi ili kupata upendeleo kwenye baadhi ya mechi, badala yake Yanga ina ongozwa kwa porojo na watu wanao ropoka ropoka hovyo, wakiambiwa watoe vithibitisho wa porojo zao wanashindwa na wakifungiwa wanaanza kutia huruma wakiomba busara za TFF, mashabiki wake wana aminishwa vitu visivyo eti watachukua ubingwa mbele ya Simba na Azam, mara Mwambusi atawapa kombe, mara Manji anarudi, ilmradi ni watu wa kudanganywa na kuota ndoto za alinacha, biashara ya jezi na kalenda imezimwa na propaganda za Haji Manara, jamaa analipwa ili kuwavuruga Yanga kuanzia uongozi hadi mashabiki, akili za watu wa Yanga zipo chini, Manara anawazidi sana, ana weza kuwavuruga na kuwafanya mpoteze uelekeo hata kama mlikuwa katika lengo sahihi, fuatilia mipango ya Yanga kutengeneza bidhaa zenye nembo ya Yanga na GSM zilivyozimwa ndani ya wiki moja kwa propaganda za Manara na baadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga wali sapoti propaganda za Manara dhidi ya uwekezaji wa GSM, lakini unajiuliza tifauti ya VUNJA BEI na GSM ni nini?. Ninachoona Yanga wana asili ya kutojiamini, ni wepesi kuvunjwa moyo, sio viongozi hata mashabiki na wachezaji pia, ukosefu wa kujiamini una sababisha afya ya akili, afya ya kimwili na afya ya kiroho ya viongozi na mashabiki pamoja na wachezaji kuwa duni, nyonge na dhaifu sana, Yanga ni timu kubwa kwa jina lakini kiuhalisia ni sawa na IHEFU FC.
Cha ajabu wachezaji hao magarasa walipokelewa kifalme walipowasili nchini kwa mara ya kwanza
DeleteNever be disappointed. Still there is a big chance because Yanga is the country's historical championship winner. Falling down is not a defeat, but a defeat is to remain where you have fallen, but still you have to find out why most such international players and coaches fail to show up with you
ReplyDeleteKuna kupambana na kupambania ubingwa aelezee vizuri hapo tafadhali
ReplyDeleteHi blog leo hawandiki goli la dube wangeshinda wao ungesikia carlino kafunga goli la video. Roha inaumwa
ReplyDeleteIngekuwa Simba kiboko ya Manula, kiboko ya Simba , goli lingezungumziwa miezi 3
Deleteuongozi una shida kabisa
ReplyDelete