April 13, 2021


 


BAADA ya Jumamosi iliyopita kushuhudia kikosi chake kikikubali kutoa sare dhidi ya KMC, Kaimu kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mwambusi amesema kuwa, bado timu yake inashindwa kutumia nafasi wanazotengeneza kuipatia mabao timu hiyo.

Yanga walitoshana nguvu na KMC katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar, bao la KMC lilifungwa na David Bryson huku la Yanga likifungwa na Yacouba Songe.

Akizungumzia hali ya kikosi chake kiufundi Mwambusi amesema kuwa sababu ya kushindwa kupata ushindi katika mchezo huo ilitokana na timu yake kutengeneza nafasi muhimu, ambazo kama wangezitumia basi wangeweza kupata ushindi na hakuna kingine.

“Timu ilicheza vizuri kwa wastani, tulikuwa na kipindi kibaya katikati ya mchezo lakini mwanzo wa mchezo na mwisho wa mchezo tulikuwa na vipindi bora na kama tungekuwa makini tungepata ushindi katika vipindi hivyo.

“Timu iliweza kutengeneza nafasi nzuri ambazo kama washambuliaji wetu wangekuwa na usahihi mzuri basi tungepata matokeo ya ushindi, tunatakiwa kuimalika zaidi ya hapa ili kuweza kukusanya pointi nyingi zaidi katika michezo ijayao,”

1 COMMENTS:

  1. Kocha mwambusi inabidi sasa umtumie said Ntibazokyiza awe mshambuliaji wa kati na sio tena kama kiungo mshambuliaji sawa ili aweze kuwa onesha akina Yacouba na Sarpong nini wanachotakiwa kukifanya over

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic