April 26, 2021


IMEELEZWA kuwa Juma Mwambusi aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesepa ndani ya Yanga baada ya kutambulishwa kwa Nassredine Nabi ambeye ni Kocha Mkuu na amepewa dili la mwaka mmoja na nusu.


Mchezo wa kwanza wa Nabi ndani ya Yanga ilikuwa jana Aprili 25 ambapo alishuhudia ubao ukisoma Yanga 0-1 Azam FC.


Mchezo wa mwisho wa Mwambusi kukaa kwenye benchi la ufundi ilikuwa ni dhidi ya Gwambina FC ambapo timu hiyo ilishinda mabao 3-1.


Mkuu wa kitengo cha Habari cha Yanga, hivi karibuni alisema kuwa bado hawajaachana na kocha huyo kwa kuwa dili lake linaishi mpaka Juni 30.


Pia kupitia Championi alieleza kuwa Mwambusi alitoa maelekezo ya mazoezi ya maandalizi ya mechi na alitarajiwa kuwa kwenye mchezo wa jana dhidi ya Azam FC jambo ambalo halikuwa hivyo.



Habari zinaeleza kuwa baada ya Nabi kutua Mwambusi alitarajiwa kuwa mshauri kwenye benchi la ufundi jambo ambalo bado halijawekwa wazi kwa sasa.

6 COMMENTS:

  1. Mwambusi hawezi kufanya kazi kama msaidizi, hawezi kuwa chini ya kocha yeyote labda awe level za gadiola and the like. Jamaa anafigisu nyingi mno na anapenda ubosi

    ReplyDelete
  2. Aende mtibwa watanatafuta kocha.Mwambusi ni kocha Mzuri.Tatizo la Yanga makocha hawapewi muda wa kuonesha uwezo wao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic