SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku.
Matola amesema kuwa wametoka kukamilisha kazi ya kusaka pointi sita kanda ya ziwa wanareja kuendelea pale ambapo waliishia.
"Tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumerejea salama kutoka kanda ya ziwa ambapo huko tulikuwa na kazi ya kusaka pointi tisa na tumezipata pia pointi hizo muhimu.
"Kiujumla kwa sasa kikosi kipo vizuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa mgumu na ushindani mkubwa, tupo tayari mashabiki watupe sapoti," amesema Matola.
Walipokutana Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ubao ulisoma Dodoma Jiji 1-2 Simba hivyo mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa ni wa kisasi.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza mechi 24 inakutana na Dodoma Jiji ambayo ipo nafasi ya 7 ina pointi 38 na imecheza mechi 27.
Akiingia huyu anasepa huyu likiondoka wimbi laingia wimbi
ReplyDeleteSimba hawatakiwi kuichukulia poa Dodoma jiji hata kidogo hapo kesho. Sababu zipo nyingi zakuwa mchezo wa kesho utakuwa wa kukamia asilimia mia mbili 200% kutoka kwa Dodoma Jiji.
ReplyDeleteSababu ya kwanza ni Uopolo.Tayari Yanga wanahangaika kutafuta sehemu ya kujiliwaza au kupozea machungu kupitia Dodoma Fc.Tayari Yanga wanahangaika kuliko wanavyohangaika Dodoma Fc kuhakikisha simba inapotoza mchezo wa kesho nadhani hata posho za wachezaji wa Dodoma fc ni Yanaga ndio walioahidi kugharamia.kwa hivyo simba tunakiwa kuwa makini sana. Ukichana na hayo Dodoma ina wachezaji kadhaa wana uwezo pia tuwe wakweli na pengine baadhi ya wachezaji wao wangetamani kuuonesha uongozi wa simba kuwa wana uwezo wa kucheza hata simba wakipewa nafasi.
Kwa upande wa fowadi ya simba bado kichefuchefu sijui tatizo liko wapi? Ni viungo ndio wanaoibeba simba kwenye magoli to be honest na ni hatari kwa timu kubwa kama simba. Fowadi ya simba inafunga ila wanapoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga magoli kuliko magoli wanayo funga by far. Boko na Kagera wamekosa kujiamini kabisa. Tunataka kuona fowadi ya simba wakipiga mashuti golini wamekuwa wakimya sana. Angalau Shabalala ameonesha vipi fowadi anatakiwa kufanya kunako mechi ya ushindani sio kuzunguka tu uwanjani No shoot on goal not harassing the backline what kind strikers?. Dube ameonesha Jana vipi fowadi anatakiwa kuchangamka ili kuipataia timu yake ushindi kunako hitajika kama fowadi tegemezi.povu ruksaa:)