April 8, 2021


 HEMED Morroco, Kocha Mkuu wa Klabu ya Namungo FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Ihefu FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa.

Ihefu kwenye msimamo ipo nafasi ya 17 ina pointi 20, inakutana na Namungo FC Iliyo nafasi ya 10 na pointi zao kibindoni ni 27.

Akizungumza na Saleh Jembe kuelekea Morocco amesema kuwa maandalizi yapo kamili na vijana wanahitaji pointi tatu.

“Haitakuwa kazi rahisi hasa ukizingatia kwamba mzunguko wa pili kila timu inahitaji pointi tatu. Mashabiki waendelee kutupa sapoti kila kitu kitakuwa sawa, tunahitaji pointi tatu” .


Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Ihefu FC, Zuber Katwila amesema:"Ni kazi kubwa kwa sasa mzunguko wa pili kutafuta matokeo, tutaingia uwanjani kwa lengo la kusaka pointi tatu," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic