April 8, 2021

 


DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa amewaambia wachezaji wake wote lazima wapambane kwenye mechi yao ya mwisho dhidi ya Al Ahly ili kuweka rekodi ya kutofungwa.

Simba imecheza jumla ya mechi 5 kwenye hatua ya makundi na imeshinda 4 na kulazimisha sare moja hivyo ndani ya dakika 450 haijapoteza na ina mchezo mmoja dhidi ya Al Ahly ambao utakamilisha dakika ya 540.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Aprili 9 nchini Misri. Walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 1-0 Al Ahly hivyo utakuwa ni mchezo wa kisasi kwa Waarabu hao wanaonolewa na Pitso Mosimane.


Akizungumza na Saleh Jembe, Gomes amesema kuwa kutinga hatua ya robo fainali wakiwa wanaongoza kundi ni heshima hivyo wanahitaji kumaliza kwa rekodi yao nzuri.

“Tumekuwa na rekodi nzuri kwenye mechi zetu za kimataifa, tunahitaji kudumu nayo muda wote, mchezo wetu wa mwisho hatua ya makundi ni dhidi ya Al Ahly hilo lipo wazi.

“Najua wametoka kupata sare mchezo wao wa mwisho dhidi ya Al Merrikh hivyo watahitaji kupata ushindi kwetu nasi tunahitaji kutokufungwa ili tuwe na rekodi bora Afrika, inawezekana,” amesema Gomes.

Kwenye kundi A ni Simba yenye pointi 13 na Al Ahly wenye pointi 8 zimetinga hatua ya robo fainali, AS Vita yenye pointi 4 itamalizana na Al Merrikh yenye pointi 2 zote zikiwa hazijafunzu hatua ya robo fainali.

Tayari kikosi cha Simba kipo nchini Misri ambapo kimeanza mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo wa kukamilisha mbio za hatua ya makundi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic