April 3, 2021


 BAADA ya jana Aprili 2, Kamati ya Maadili ya Shirikisho la  Mpira wa Miguu, Tanzania, (TFF) kummfungia miaka mitano Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kujishughulisha na masuala ya mpira wa miguu ndani na nje ya nchi, kiongozi huyo amesema kuwa alijua ingekuwa hivyo.


Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TFF Aprili 2 imeeleza kuwa kamati imemkuta na hatia ya kutoa maneno ya uchochezi kwa Wanachama na mashabiki kuhusu vyombo vinavyosimamia mpira.

Mwakalebela amesema kuwa ameambiwa kwamba asijihusishe na masuala yoyote yanayohusu michezo.

"Nimeambiwa nisijihusishe na masuala yoyote yale yanayohusu michezo, yaani iwe kwenye magazeti ya michezo nimeambiwa nisisome hata magazeti ya michezo.

"Ikiwa ninatazama TV ikifika wakati wa michezo nisiangalie, niliwaambia viongozi wangu kwa namna mwenendo ulivyokuwa basi ningefungiwa kwa namna mambo ambavyo yalikuwa yanakwenda.

"Nimekuwa nikiitetea Yanga katika masuala ya michezo na kila ambacho nimekuwa nikifanya ni kwa sababu ya Klabu ya Yanga,".

4 COMMENTS:

  1. ndiyo uwezo wake wakufikiria umeiishia hapo. kama yuko nyumbani kwake akitaka akisoma gazeti ikifikia kurasa za michezo aache kusoma..kama anaangalia TV azime ikifika kwenye michezo...hukumu maana yake ni kutokujihusisha in public kama alivyokuwa akikurupuka kila mara morrison akitoa asist au kufunga goli..safi sana TFF

    ReplyDelete
  2. basi Yanga wakuteetee sasa

    ReplyDelete
  3. Huo ni upotoshaji, utazuiwaje kusoma na kuangalia michezo? Labda amezuiwa kuandika makala kwenye magazeti au kufanya tv coverage kuhusu mpira wa miguu.

    ReplyDelete
  4. Alionywa na wanaomrqkia kheri lakini ndo hivo. Usituhumu bila kuwa na ushahidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic