KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, amefunguka kuwa straika wa timu hiyo, Prince Dube ana nafasi kubwa ya kutwaa Tuzo ya Ufungaji Bora Ligi Kuu Bara msimu huu kutokana na kasi yake ya ufungaji.
Dube raia wa Zimbabwe, alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa 2-0 walioupata juzi Ijumaa dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo uliopigwa Dimba la Azam Complex, Dar.
Mabao hayo yamemfanya Dube kufikisha kumi akiwa kinara akiwazidi washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na John Bocco ambao awali walikuwa wakiongoza kila mmoja akifunga mabao tisa.
Akizungumza na Spoti Xtra, Bahati raia wa Burundi, amesema:-“Dube ni mchezaji mzuri ninafurahishwa na kiwango chake, tangu apone majeraha yake amekuwa kwenye kiwango bora, kwa uwezo ambao ameendelea kuuonesha kwa kiasi kikubwa ana nafasi ya kutwaa Tuzo ya Ufungaji Bora.”
labda awe anashindana na Sarpong na Nchimbi
ReplyDelete