April 22, 2021

 


BAADA ya Klabu ya Raja Casablanca ya Morocco kusepa na pointi tatu mbele ya Namungo FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, timu hiyo imewashukuru Watanzania kwa ukarimu wao.

Mchezo huo uliochezwa jana Aprili,21 Uwanja wa Mkapa Namungo ya Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Seleman iliokota mabao matatu nyavuni huku lango la wapinzani likiwa salama dakika zote 90.

Ni Illias Haddad alipachika bao dakika ya 9, Fabrice Ngoma alipachika la pili dakika ya 14 na msumari wa mwisho ulipachikwa na Zakaria Habti dakika ya 36.

Mohamed Bekkari, Kocha  wa Raja Casablanca amesema kuwa anafurahi kuwa Tanzania na namna ambavyo watu wake wamekuwa ni wakarimu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bekkari amesema kuwa wanafurahi kwa kuwa wampeta pointi tatu pamoja na huduma nzuri walizopata baada ya kuwa Tanzania.

"Imekuwa furaha kwetu kupata pointi tatu na hatujapoteza mchezo, kikubwa ni furaha na tunawashukuru Watanzania kwa sapoti yao pamoja na ukarimu," .

Katika kundi D kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho,  Raja Casablanca inaongoza kundi ikiwa na pointi 15 baada ya kushinda mechi zote tano na Namungo ipo nafasi ya 4 ikiwa haijakusanya pointi. 

4 COMMENTS:

  1. Unajua CCM ndiyo akili zetu ,ukweli Namungo haikupaswa kucheza Ligi,kwa mujibu wa TFF na Thiiimba ila ukweli na uzuri wote ni wale wale KARIA,WASIOJALiWa ,KASSoNGo Na JND zaidi tulia ukamatwe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unatumia ubongo gani kuwaza?Wa kichwani au wa makalioni?Namungo walipambana hadi kufika fainali ya FA na kustahili kupata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye kombe la shirikisho halafu wewe unakuja na maoni ya hovyo utadhani umetoka kuzimu leo.Ulitaka nani awakilishe wakati walishindwa kupata hiyo nafasi uwanjani

      Delete
  2. Utoporo situliwapiga 4g mkashindwa kufika fainali iweje muwalaumu namungo? Ambayo hatukuifunga nne fainali. Ukizungumzia kimataifa ni simba na namungo tu

    ReplyDelete
  3. Hii ni Yanga au Takataka hahahhaaa
    Hii ni Yanga au Utopoloooo 😄😄😃😃😂😂😂😂😂

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic