April 22, 2021

 


KIKOSI cha Ruvu Shooting kinachonolewa na Kocha Mkuu, Charles Mkwasa kimewashushia kichapo cha mabao 5-1Mwadui FC na kuzidi kuzamisha matumaini ya timu hiyo kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.


Ni Edward Manyama alifungua pazi la mabao dakika ya 17 na Shaban Msalla akapachika mabao mawili ilikuwa dakika ya 37 na 82, Richard yeye alipachika moja dakika ya 48 sawa  na Abrahaman Mussa aliyepachila bao dakika ya 76.


Bao pekee la Mwadui FC lilipachikwa na Mohamed Hashim dakika ya 57 ilikuwa Uwanja Mabatini yalipo maskani ya Ruvu Shooting. 


Ushindi huo unaifanya Ruvu Shooting kufikisha jumla ya pointi 37 ikiwa nafasi ya 6 huku Mwadui ikibaki na pointi 16 nafasi ya 18 kwenye msimamo

2 COMMENTS:

  1. Simba mnajipangia mechi nyepesi mnakimbia mechi ngumu lkn mimba huwa inatoka kawaida au operation mmemaliza wepesi Sasa tunawasubiri

    ReplyDelete
  2. Vipi mbona Utopolo unateseka.Huoni ajabu bodi ya ligi inawapangia mechi Utopolo ili mzidi kuongoza ligi baada ya kuacha Simva imalize mechi zake.Hizo mechi ngumu ni zipi?Mmeanza kuweweseka sasa baada ya kufikiwa.Mnapangiwa mechi na muda wa kupumzika. Chukulia mfano mechi ya Jumapili na Azam mnapumzika siku 4 wakati Azam anacheza leo na kucheza tena Jumapilisiku 2 za mapumziko.Simba amecheza na atacheza kila baada ya siku 2.
    Mbona safari hii hamlalamiki kuhusu viporo au mahesabu yamegoma?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic