April 18, 2021


 REAL Madrid inaripotiwa kwamba ipo kwenye mpango wa kumuuza nyota wake Gareth Bale ili kupata mkwanja kwa ajili ya kufanya usajili.

Real Madrid inapambana kuisaka saini ya nyota wa Borrusia Dortmund,  Erling Haalad.

Haalad pia anapigiwa hesabu na Manchester United, Chelsea ambazo nazo pia zinahitaji saini yake.

Kwa sasa Bale yupo zake kwa mkopo ndani ya kikosi cha Tottenham kinachoshiriki Ligi Kuu England.

Nyota huyo aliweka wazi kwamba anahitaji kurejea Real Madrid kuendelea kupambania namba pale muda wake wa mkopo ukiisha ila kwa hali ilivyo huenda asirejee.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic