April 5, 2021

 


JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kurejea kwa Saido Ntibanzokiza kumeongeza ari ya kupambana kwa kikosi hicho ambacho kinaongoza Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Kikiwa kimecheza jumla ya mechi 23 kwenye ligi kimekusanya jumla ya pointi 50 kinafuatiwa kwa ukaribu na watani zao wa jadi Simba wenye pointi 46 nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 20. 

Kiungo huyo mshambuliaji raia wa Burundi alikuwa nje ya uwanjakutokana na kuwa na majeraha ya aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons na alijitonesha tena alipocheza na Simba kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi. Alipopona alijiunga na timu ya taifa ya Burundi kuwania kusaka tiketi ya kufuzu Afcon.

Tayari ndoto ya Burundi kufuzu Afcon imeyeyuka kama majirani zao Tanzania hivyo amerejea kuendelea na kazi ndani ya kikosi cha Yanga.

Mwambusi amesema:"Saido amerejea na hivyo anaongeza idadi ya wachezaji ambao wanaendelea kufanya mazoezi pamoja na ni faraja kwetu kwa kuwa tunaamini kwamba amepona na amekuja kuendelea kufanya kazi,".

Mchezo unaofuata kwa Yanga kwenye ligi ni dhidi ya KMC unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 10 baada ya ligi kusimama kutokana na maombolezo ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli.

Ikiwa atakuwa fiti zaidi huenda atakuwa sehemu ya kikosi kitakachovaana na Wanakino Boys ambao walipokutana nao kule Mwanza, Uwanja wa CCM Kirumba, ubao ulisoma KMC 1-2 Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic