April 22, 2021

 


MICHAEL Sarpong, mshambuliaji wa kikosi cha Yanga raia wa Ghana ametimiza siku 136 ambazo ni sawa na saa 3,264 za kucheza bila kufunga bao kwenye mechi zote za ushindani ikiwa ni zile za Ligi Kuu Bara na Shirikisho.

Kwenye ligi Yanga ina pointi 57 baada ya kucheza mechi 26 na ina mabao 41 amehusika kwenye mabao 7, alifunga mabao manne, pasi mbili za mabao na alisababisha penalti moja kwenye mchezo dhidi ya KMC, Uwanja wa CCM Kirumba.

Ukurasa wa mabao alifungua Uwanja wa Mkapa wakati ubao ukisoma Yanga 1-1 Tanzania Prisons, ilikuwa ni Septemba 6 kisha Oktoba 31 akawatungua Biashara United, Uwanja wa Karume. Novemba 7 akawatungua Simba ilikuwa ni kwa mkwaju wa penalti na Desemba 6 alifunga akaunti yake ya mabao kwa kuwafunga Ruvu Shooting ilikuwa Uwanja wa Mkapa.

Nyota huyo hivi karibuni alisema kuwa anatambua kwamba mashabiki wanahitaji kumuona akifunga jambo ambalo anapenda kuona likitokea.

Wakati ubao ukisoma Yanga 3-1 Gwambina, Uwanja wa Mkapa alimpa pasi mshikaji wake Said Ntibanzokiza.

3 COMMENTS:

  1. Mmeanza sasa Kwani Ajibu Ana siku ngapi hajafunga? Kwani Chikwende na Morrison wana siku ngapi hawajafunga?

    ReplyDelete
  2. Ajibu na Morrison sio first 11 ya Simba,chikwende Hana hata miez miwili unamuhesabia wa nin?ukweli unauma sana,sapong wenzake ni kagere,boco,mugalu,hapo hakuna mchezaji ni garasa hilo.

    ReplyDelete
  3. Uto msijali, hata asipofunga kwani kuna shida gani... Kikubwa ana mikimbio mingi basi anafaa kuendelea kuwepo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic