April 23, 2021


 SELEMANI Matola, Kocha Msaidizi wa Simba,

amesema kuwa wanapata tabu kupanga kikosi

cha kwanza kutokana na ubora wa wachezaji

wote walionao kikosini.


Simba ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara

wakipambana na watani zao wa jadi, Yanga

ambao wapo nafasi ya kwanza na pointi zao 57 huku wao Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi 55.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola

amesema kuwa kitu ambacho kinalichanganya

benchi la ufundi la Simba ni katika kupanga

kikosi cha kwanza.


“Tuna wachezaji wazuri ndani ya kikosi cha

Simba jambo hilo linatufanya tuwe tunapata

tabu kwenye kupanga kikosi cha kwanza, hii

inatokana na wachezaji wetu wote kuwa bora.


“Kuanzia Chama, (Clatous) Jonas (Mkude), Luis, (Miqiussone) John

(Bocco), Morrison (Bernard) hawa wote ni

wachezaji wazuri sasa wakati wa kupanga kikosi

cha kwanza huwa tunapata tabu na hili

linatuchanganya.


“Ila yote haya ni muhimu kuweza kufanya vizuri

kwa sababu ili uweze kupata matokeo mazuri ni

lazima uwe na kikosi kizuri na chenye wachezaji

bora, hicho ndicho kinachofanya tufanye

vizuri,” amesema Matola.

Mechi mbili wakiwa nje ya Dar wameweza kukusanya pointi sita na mabao matatu huku ngome yao ya ulinzi ikiwa haijaruhusu bao.

Ilishinda kwa tabu mbele ya Mwadui FC hii ni kwa mujibu wa Matola, pale ubao uliposoma Mwadui 0-1 Simba na Kagera Sugar 0-2 Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic