KAMPUNI
ya michezo ya kubashiri SportPesa imemkabidhi rasmi mshindi wa awamu ya sita wa
Jackpot mfano wa hundi ikiwa ishara ya kutimiza wajibu kama kampuni kwa
washindi wake na ameweka wazi kwamba yeye ni shabiki wa Klabu ya Yanga kwa Tanzania na Ulaya ni Manchester United.
Mkazi wa
Tabora-Sikonge Abdulaziz Ibrahim, (24)
ambaye pia ni mwajiriwa wa duka la dawa na maabara amekabidhiwa na SportPesa
pesa aliyoshinda Jackpot ya mechi 13. Wakati wa makabidhiano katika ofisi za
SportPesa Abdulaziz amesema “Nafurahi sana kwani baada ya kusubiri kwa kipindi
kilichopangwa leo nimekabidhiwa rasmi fedha zangu.
“Napenda
kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu kwa kuniongoza maana
nilishajaribu mara kadhaa lakini sikufanikiwa.
“Siku
niliyoshinda niliweka mikeka kumi na kila mmoja shilingi elfu mbili, katika
mikeka yote 10 mkeka namba 7 ndio niliofanikiwa kushinda kwa mechi zote.
“Mimi ni
shabiki mkubwa wa Manchester United na kwa hapa Tanzania nashabikia Young
Africans.(Yanga) Siku niliyoweka mikeka yangu niliikosesha ushindi Man U ambayo
ilikuwa inacheza na Leicester City kupelekea kufanikisha vizuri ushindi wangu,”
alisema Abdulaziz.
Kwa
upande wa SportPesa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tarimba Abbas alianza kwa
kuwashukuru Waandishi wa Habari kwa kuhudhuria tukio hilo muhimu la kumkabidhi
mshindi mfano wa hundi ya shilingi 521,471,360 na kusema kuwa;
“Leo ni
siku ambayo tulikuwa tunaingojea kwa hamu sana maana tumeweza kukamilisha hili
zoezi, huyu mshindi alipatikana tangu tarehe Machi 22, mwaka huu lakini ilibidi
tusubiri kipindi hiki cha maombolezo kimalizike ndipo tuendelee na sherehe ya
kumkabidhi.
“Katika
ushindi wake Abdulaziz ameweza kubaki na Shilingi 417,177,488 huku akitoa
Shilingi 104,293,872 kama malipo ya kodi ya zuio.
“Lengo
letu ni kuendelea kuwainua vijana Wakitanzania na kuhakikisha tunabadilisha
maisha yao, kwa kucheza jackpot tumeweza kuona jinsi Abdulaziz anavyoenda
kubadili maisha yake.
“Kila
siku tunaendelea kuwa wabunifu ili kuhakikisha tunaboresha huduma na kuwafanya
wateja wetu wazidi kufurahia kucheza na SportPesa.
“Hivi
sasa Jackpot yetu imepanda upya na kufikia kiasi cha shilingi TZS 218,361,140
ambapo kwa atakayebashiri kwa usahihi mechi 13 ataibuka mshindi na kwa
watakaobarishi kwa usahihi kuanzia mechi 10 hadi 12 watapata bonasi ya wiki.
“Endapo
Jackpot haitopata mshindi kwa wiki hiyo huongezwa mpaka pale mshindi
atakapopatikana,” amesema Tarimba.
Good
ReplyDelete