MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Prince Dube amesema kuwa bao lake ambalo alifunga mbele ya Yanga ni maalumu kwa ajili ya timu yake, pia ameongeza kwa kusema kwamba yeye ni mchezaji wa Azam kwa sasa hawezi kufikira kuhusu timu nyingine.
Kwa upande wa ligi ya Tanzania amesema kuwa anawashukuru kwa sapoti ambayo wanampa jambo linalompa furaha. Dube kwa sasa ni namba moja kwenye utupiaji akiwa amefunga jumla ya mabao 12 ndani ya ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment