April 24, 2021




 IKIWA leo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes inatarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya Gwambina FC imeweka wazi kwamba Uwanja wa Gwambina Complex sio rafiki kwao.

Sababu hii pia ilitajwa wakati wakipata ushindi kwa tabu mbele ya Mwadui FC baada ya ubao kusoma Mwadui 0-1 Simba bao lililopachikwa na John Bocco dakika ya 66.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanatambua utakuwa mchezo mgumu ila sehemu ambayo wanachezea sio rafiki.

"Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Gwambina ila tunatambua kwamba hautakuwa mchezo mwepesi hilo lipo wazi lakini uwanja kwetu sio rafiki.

"Tutajitajihidi kufanya vizuri tumeona sehemu ya kuchezea sio nzuri lakini hakuna namna ni lazima tupambane ili kupata matokeo chanya," amesema.

Kwenye msimamo wa ligi, Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 55 baada ya kucheza mechi 23 inakutana na Gwambina FC iliyo nafasi ya 12 na pointi 30.

 

5 COMMENTS:

  1. Uandishi maandazi unaleta ushabiki mbele ya kazi

    ReplyDelete
  2. Asilimia kubwa waandishi hawapendi Simba na mara zote wanazungumza utumbo lakini Simba ndo ipo juu

    ReplyDelete
  3. Mara kwani mara shabalala mara kichuya alimradi kututoa penye tell pumbaacu

    ReplyDelete
  4. Mara chama mara kagere ukitaka kujua Simba muulize yule kocha wa gwambina wanazungumza facts na ule ushindi wa yanga kwa gwambina ni pumbavu wa kipa hakuna goli la ufundi pale

    ReplyDelete
  5. Wewe kwa macho yako uaona huo ni uwanja Bora. Ushabiki unadumaza taaluma. Pole Sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic