April 13, 2021

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Malota Soma ‘Ball Jagler’ amesema kuwa anaiona Simba ikiwa na uwezo wa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika endepo timu hiyo itajitoa zaidi mara baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Malota Soma ni moja kati ya wachezaji wa Simba ambao waliunda kikosi cha Simba kilichotinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 1993 na kufungwa na klabu ya Stella Abdjan.

Akizungumzia kiwango cha Simba, Malota amesema kuwa mara baada ya Simba kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali, hatua inayofuata inahitaji utulivu na kujituma jambo ambalo kama Simba watakuwa makini nalo basi wanaweza kuwa mabingwa.

“Simba imelionyesha bara zima la Afrika kuwa ni moja kati ya timu kubwa na tishio kwa sasa,kutinga hatu ya robo fainali si jambo jepesi kwani kuna timu nyingi hazijafikia walipofika Simba na ni timu kubwa hapa Afrika.

“Hivyo kama Simba watacheza michezo inayofuata kwa nidhamu kubwa na kujitolea kwa moyo wote basi wanaweza kutwaa ubingwa msimu huu kwani timu nyingi zilizofuzu robo fainali hazina ubora kama wa Simba,” amesema mshambuliaji huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic